KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 23, 2013

Angel Di Maria amesema haoni sababu ya kumkimbia Messi Real Madrid

Angel Di Maria amesema kuwa alijua kuwa kuwasili kwa Gareth Bale ndani ya Real Madrid kungeleta kitu kipya ndani ya klabu hiyo lakini amekanusha taarifa ya kuwa anataka kuihama klabu hiyo
Tangu kuwasili  kwa Bale mwezi Septemba kwa uhamisho wa rekodi wa euro milioni €100 kumeibuka maswali mengi huku hoja zikisema kuwa hadhi ya Di Maria ndani ya los Blancos imeshuka na kwamba anafikiria kuondoka Bernabeu.

Di Maria ambaye alifunga goli na kutoa pasi ya mwisho katika mchezo wa Madrid wa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Valencia, amesema alitegemea kucheza michezo pungufu lakini amekanusha taarifa kuwa anajipanga kusaka muelekeo mwingine.
“Nilijuwa kuwa mshambuliaji huyo kasajiliwa kwa hela nyingi euro milioni €100 na lazima achezeshwe” .

“Hapana sijaomba kuondoka. mawazo yangu ni Real Madrid. we mwandishi ulie andika kuwa nakwenda Tottenham au klabu nyingine hizo taarifa umezipata wapi."

Di Maria amecheza michezo 15 kati ya michezo 17 ya kikosi cha Carlo Ancelotti msimu huu.

No comments:

Post a Comment