KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 20, 2013

Breaking news: Suarez aongeza mkataba na Liverpool na kumaliza tetesi za kuihama mwezi Januari

Luis Suarez amesaini mkataba wa kipindi kirefu na Liverpool
Luis Suarez amemaliza tetezi za juu ya hatima yake ya baadaye kufuatia kuongeza kandarasi yake ya muda mrefu ndani ya Anfield.
Liverpool imethibitisha hilo hii leo kuwa mfungaji wao huyo Mruguay ambeye ameshatikisa nyavu mara 17 mpaka sasa msimu huu ameingia mkataba mwingine wa kumaliza ubishi juu ya hatma yake ya baadaye.
 
Mwenyewe Suarez amenukuliwa akisema
‘ninafuraha kukubaliana kwa mpango mwingine na Liverpool na hatama yangu ya baadaye kuwa katika hali ya salama kwa kipindi kirefu.

Speculation: Suarez had asked for a transfer during the summer but Friday's news ends speculation he'll be leaving the club in January
Tetesi: Suarez alitaka kuondoka kipindi cha uhamisho cha majira ya kiangazi lakini habari za Ijumaa ya leo zimemaliza tetesi hizo za kwamba angeondoka katika klabu hiyo mwezi Januari.

‘Tuna wachezaji kadhaa wakubwa na timu inaimarika muda wote. Naamini nitafanikisha malengo ya kushinda mataji na kucheza katika kiwango cha juu nikiwa na Liverpool. Madhumuni yangu ni kuiwezesha kufika kule haraka iwezekanavyo.
 
‘Haina ubishi moyo ninaonyeshwa na mashabiki wa Liverpool inanitia moyo. Najivunia kuwawakilisha na kufanya vema kwa kadri ya uwezo wangu kila mara ninapo vaa jezi.
 
‘Ninamahisinao mazuri wananionyesha mapenzi na mimi pia nawapenda. Mara zote nitajitahidi kuwafanyia vizuri na nina matumaini tutafanikiwa pamoja.’
 
Meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers naye amekaririwa akisema
‘Hizi ni habari njema kwa kila mtu anayehusika na klabu, timu, wamiliki na zaidi washabiki.
'Luis ni kipaji cha kiwango cha dunia na kuongeza mkataba wa kuendelea kutoa huduma hapa ni muhimu kwakuwa tunajaribu kufikia mafanikio.
'Muhimu zaidi na cha kufurahisha ni kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 mafanikio makubwa zaidi kwake ni miaka ijayo na tunajua sasa kuwa tutashuhudia mafanikio hayo akiwa na jezi ya Liverpool
In form: Suarez scored twice as Liverpool enjoyed a 5-0 win at Spurs on Sunday
Kiwango: Suarez alifunga magoli mawili katika mchezo ambao Liverpool iliifunga Spurs bao 5-0 Jumapili iliyopita.