KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 12, 2013

Javier Zanetti anamlilia Ezequel Lavezzi ndani Inter Milan

 Javier Zanetti amesema angependelea kuwa siku moja inapatikana nafasi ya kucheza pamoja na Ezequel Lavezzi ndani ya klabu ya Inter Milan.

Mshambuliaji huyo wa Argentina amekuwa akihusishwa mno kuelekea Nerazzurri kufuatia kutokuwa katika kiwango kizuri msimu huu baada ya kusajiliwa Edinson Cavani ndani ya Paris Saint-Germain kwa euro milioni €64.

Licha ya kwamba anapiga kuimarisha kiwango chake kwa mabingwa hao wa ligi ya Ufaransa ya Ligue 1 mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anafikria njia ya kurejea tena katika ligi ya Italia Seria A na huwenda akafanikiwa mwezi Januari ambapo Zanetti atakuwa ni chagizo kubwa kwa kikosi cha Walter Mazzarri.

"tunapo mzungumzia Lavezzi, tunazungumza habari ya bingwa ambaye tungependa kuwa naye ambaye timu nyingi wanapenda kupata huduma yake" amesema Zanetti.

"kocha ataamua na kutolea maelezo nini kitakuwa bora kwa timu"

Inter imeshinda mchezo mmoja tu katika michezo minne iliyopita ya Serie A baada ya kuanza vizuri kampeni ya msimu huu na sasa wanakabiliana na Napoli na AC Milan katika derby ya majira ya baridi.

Zanetti anadhani kikosi kinaweza kuwatumia wachezaji wake waliokuwa majeruhi kwa michezo hiyo muhimu akiwemo Mauro Icardi.

"kitu kizuri ni kwamba Mauro amepona ni muhimu kikosini " anasema Zanetti. lakini kuhusu Diego Milito anasema kuwa huenda yeye na Walter Samuel wakarejea kwa derby hiyo.

No comments:

Post a Comment