Mlinda mlango wa Zambia Chipolopolo Joshua Titima ameibuka shujaa katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa michuano ya chalenji ya CECAFA 2013 na kuwapa nafasi hiyo timu hiyo aalikwa, kufuatia kudaka peneti ya nahodha wa kikosi cha Kilimanjaro Star, Kelvin Yondani ambapo mbali na ushindi huo pia kikosi hicho kimezawadiwa dolari za kimarekani 10,000.
Mchezo huo ulifikia katika kipindi cha kupigiana penati baada ya kukamilisha dakika 90 za kawaida za mchezo kwa sare ya bao 1-1 huku Zambia wakiwa wakiwa wa kwanza kuandika bao dakika 7 tu baada ya mapumziko kupitia kwa Ronald Kampamba likiwa ni goli lake la pili ndani ya mashindano hayo.
Hata hivyo mshambuliaji wa TP Mazembe ya DR Congo alidhihirisha ubora wake na uhalali wake wa kuwepo katika orodha ya kuwania tuzo ya ubora Afrika kwa wachezaji wanao chezea soka Afrika 2013 kwa kufunga goli safi kwa guu la kushoto.
Katika kupigiana penati wachezaji wa Kilimajaro waliokosa penati zao ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa and Kelvin Yondani wakati ambapo kwa upande wa Chipolopolo waliokosa ni Mtonga Kondwani na Justin Zulu.
Wafungaji wa penati wa Kilimajaro Stars walikuwa ni Mbwana Samata, Erasto Nyoni, Himidi Mao Mkami , Amri Kiemba Ramadhani Yahaya Singano kwa Upande wa Zambia
walikuwa ni Felix Katongo, Ronald Kampamba, nahodha Bronson Chama, Julius Situmbeko, Rodrick Kabwe na Kabaso Chongo.
Tanzania XI :
Ivo Phillip Mapunda (GK), Kelvin Yondani (capt), Erasto Edward Nyoni, Pius Michael Aidan, Said Hussein Moradi, Idd Athuman, Abubaker Salum, Saleh Dilunga, Alfan Ngasa Mwrisho, Ally Mbwana Samata and Kiemba Ramadhan.

Zambia XI:
Joshua Titima, Bronson Chama (capt), Jimmy Chisenga, Rodrick Kabwe, Kondwani Mtonga, Sydney Kalume, Alex N'gonga, Jistin Zulu, Festus Ndewe, Ronald Kampamba and Felix Katongo
Coach: Patrice Beaumelle
Joshua Titima, Bronson Chama (capt), Jimmy Chisenga, Rodrick Kabwe, Kondwani Mtonga, Sydney Kalume, Alex N'gonga, Jistin Zulu, Festus Ndewe, Ronald Kampamba and Felix Katongo
Coach: Patrice Beaumelle
Match Officials: Mutaz Khairala (Sudan)-center referee, Gilbert
Cheruiyot (Kenya)-1st assistant, Simba Honore (Rwanda)-2nd assistant,
Richard Gahunzire (Rwanda)-Match Commissioner, Ali Ahmed (Somalia) -
Referees' Inspector
No comments:
Post a Comment