![]() |
Benchi la ufundi la Azam kushoto ni Kalimangonga Ongala na Joseph Omog |
Ratiba ya michezo ya vilabu barani Afrika hususani kombe la shirikisho iliyotolewa jana na shirikisho la soka barani Afrika CAF ni wazi kabisa kuwa haimnyimi usingizi kocha mpya wa Azam fc ya Tanzania Mcameroon Joseph Marius Omog ambaye amechukua mikoba ya mwingereza Stewart John Hall kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa ratiba ya CAF ya michuano ya kombe la shirikisho ni kwamba Azam fc itaanzia ugenini dhidi ya Ferreviario De Beira ya Mozambique mchezo ambao bila shaka utafanyika huko Beira.
Hii ni ratiba nyepesi ya kuanzia kwa upande wa Azam fc ambao huu kwao ni msimu wa pili mfululizo wanashiriki michuano hii ya vilabu barani Afrika.
Itakumbukwa msimu wa mwaka 2012/2013 Azam ambayo ilikuwa ikiingia kwenye uzoefu mpya wa michuano ya vilabu barani Afrika waliaanza na Al Nasri Juba ya Sudan Kusini jijini Dar es Salaam ilikuwa ni tarehe 16/02/2013 na Azam waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 huku mabao hayo yakifungwa na Abdi Kassim 'Babi' na Kipre Tchetche kabla ya kuikandamiza tena katika uwanja wa ugenini katika mchezo wa marudiano kwa mabao 5-0 yaliyofungwa na Hamisi Mcha Vialli mabao 3 Hat-trick , John Boko na Salum Abubakar 'sureboy'.
Azam ilipita na kutinga roundi ya pili kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1.
Umony wa Azam akimpongeza Babi kwa kumshika kichwa baada ya kufunga goli dhidi ya Al Nasri Juba |
Katika raundi ya pili Azam fc ilikutana dhidi ya Barrack Y.C 11 ya Liberia ambapo mchezo wa kwanza ilichezwa tarehe 17/03/2013 nchini Liberia ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Humphrey Mieno na Seif Abdalah 'Karihe' kabla ya mchezo wa marudiano uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salam tarehe 05/04/2013 ambao ulimazika kwa suluhu 0-0, ambayo iliiwezesha Azam fc kutinga hatua iliyofuata ya ikipangiwa kucheza dhidi ya Waarabu wa FAR Rabat ya Morocco, ambapo walikwenda suluhu 0-0 mchezo wa kwanza uwanja wa Taifa kabla ya kupokea kichapo cha bao 2-1 ugenini Rabat na kumaliza safari yao ya michuano hiyo.
Kwanini nilianza kwa kusema ratiba iliyotoka hamnyimi usingizi, ni kwasababu kocha huyu mwenye umri wa miaka 42 ana uzoefu mkubwa na mashindano ya vilabu Afrika, achilia mbali kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon ya wachezaji wa ndani CHAN 'Indomitable
Lions' lakini pia kwa upande wa vilabu alifanya vema akiwa na AC Leopards ambao ni vigogo wa soka nchini Congo Brazaville.
Imani kubwa hapa ni kwakuwa Azam fc tayari imesha pata uzoefu kwenye michuano ya vilabu Afrika na ilipoishia msimu uliopita si haba, lakini pia kwa kuwa na kocha mwenye uzoefu mkubwa wa kiwango hiki katika klabu hii ambayo imekuwa na miundo mbinu yakinifu ya kisoka yenye mwelekeo wa kubadili utamaduni hasi uliozoeleka wa soka la Tanzania lisilo kuwa la uwekezaji, isipokuwa porojo na fitna, basi huenda wakadhihirisha hilo katika michuano ijayo ya vilabu Afrika wakiwakilisha kwa mara ya pili katika michuano ya kombe la shirikisho.
Mafanikio ya Joseph Marius Omog kuiwezesha AC Leopards ya Congo Brazaville kutwaa mara mbili taji la ligi ya soka ya nchi hiyo na kuweka histori kubwa barani Afrika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 38 kupeleka taji la michuano ya kombe la Shirikisho nchini Congo, hiyo yatosha Azam fc Kujivunia kuwa na kocha mwenye kaliba kama hiyo klabuni hapo kama kocha mkuu.
AC Leopards iliichapa Djoiba ya Mali ushindi wa jumla wa mabao 4-3 uliotokana na sare ya mabao 2-2 ugenini mjini Bamako kabla ya kuwafunga 2-1 mjini Brazaville.
Sifa kubwa ya makocha ni kutwaa makombe kama ilivyo kwa Omog ambaye tayari ameshavaa zawadi kubwa ya ubingwa barani Afrika na hivyo kumfanya kunywa maji ya baridi yenye barafu huku akisikilizia raha ya ubaridi wake kooni kwani ratiba yake ya mchezo wa kwanza ni nyepesi.
Ni wazi kuwa katika michuano iliyopita ya vilabu Afrika timu kutoka Mozambique Liga Muculmana iliwafungisha virago Gaboroni United ya Botswana kwa ushindi wa mabao 3-2 katika hatua ya awali ilhali timu ya Gaboroni United ni moja kati ya timu nzuri ukanda wa kusini mwa Afrika.
Baadaye tena katika raundi ya pili Muculumana iliwafungisha virago Lobi Stars ya Nigeria kwa mabao mengi ya ushindi wa jumla wa 8-4 baada ya ushindi wa kushangaza wa mabao 7-1 katika mchezo wa pili wa marudiano.
Ni wazi kuwa soka la msumbiji kwa kiwango cha vilabu si baya sana lakini uzoefu wa kocha Joseph Marius Omog ni chachu ya kuiwezesha Azam fc kuwadhoofisha wapinzani wao Ferreviario de Beira ya Mozambique katika mchezo wa raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho barani Africa.
Mungu ibariki Azam fc.
No comments:
Post a Comment