![]() |
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere akionekana dhahiri akionyesha dhihaka ya kidole cha kati uwanjani Etihad
|
Jack Wilshere wa Arsenal amekutana na adhabu ya chama cha soka nchini England (FA) ya kusimama mchezo mmoja, kufuatia kuonyesha dhihaka ya dole la kati kwa mashabiki wa Manchester City wakati wa mchezo waliopoteza kwa kichapo takatifu cha mabao 6-3 mchezo ulichezwa katika dimba la ugenini la Etihad.
Chama cha soka cha England kimepitia taarifa ya mchezo mzima ya mwamuzi Martin
Atkinson kabla ya kuzindua kusikiliza kesi dhidi ya Wilshere
kufuatia picha za televisheni kumuonyesha akiinua kidole cha kati kuelekea kwa mashabiki wa timu mwenyeji.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hapo kabla alikaririwa akisema klabu yake itakubaliana na adhabu hiyo ya FA kwa kiungo wake.
Wilshere amepewa mpaka kesho jioni kutoa neno lolote kuhusiana na adhabu hiyo.
Taarifa ya FA imesomeka
'Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ameadhibiwa na FA kwa kosa la kutukana kwa kutumia dhihaka.
'Adhabu inakuja kufuatia kuyonyesha dhihaka hiyo wakati wa mchezo baina ya Manchester City na Arsenal uliochezwa uwanja wa Etihad Jumamosi ya Disemba 14. Tukio hilo halikuonwa na waamuzi wa mchezo lakini ni kwa kupitia video ya mchezo husika.
'Wilshere amehadhibiwa wakati huu ambapo FA ikiwa chini ya mradi wake wa kupiga vita matukio yasiyokuwa yakistaarabu uwanjani katika michezo ya Premier League.
'katika mpango wa sasa wa FA endapo kuna tukio lolote ambalo halikuonekana na waamuzi, timu ya watu watatu itaundwa na FA kupitia tukio husika na na kusahauri kwa tukio ambalo pengine mwamuzi alipaswa kutolea maamuzi kwa wakati husika.

Wilshere hakuwa katika kiwango kizuri siku ya tukio mchezo uliochezwa Etihad
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez aliwahi kufungiwa mchezo mmoja na kipigwa faini ya pauni £20,000 na kisha kuonywa kutokufanya hivyo hapo baadaye kufuatia dhidhaka kuelekea kwa mashabiki wa uwanja wa nyumbani wakati akitoka uwanjani katika mchezo wa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Fulham Disemba 2011.

Euro 2000: David Beckham akiwa kijana alionyesha dhihaka ya kidole cha kati kwa mashabiki baada ya kichapo cha timu ya taifa ya England kutoka kwa Ureno cha mabao 3-2

Huko nyuma Luis Suarez wa Liverpool alionyesha dole la kati kwa mashabiki wa Fulham na kisha kusimamishwa kwa mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment