- Historia inasema vilabu saba viliingia msimu wa krismass wakiwa vinara na kisha kutwaa taji.
- Chelsea imeingia katika msimu kama huu na kuwa wa kwanza mara tatu, Arsenal mara mbili
- Sunderland, ndiyo klabu pekee iliyoingia katika msimu huu wakishika mkia lakini walifanikiwa kusalia katika ligi.
Mbanano ni mkubwa katika sehemu ya juu katika msimamo wa ligi ya nchini England katika kipindi hiki cha msimu wa Krismass huku kila timu ikitaka kumaliza katika usukani wa ligi hiyo na Arsenal wanaonekana kuangaziwa zaidi na miale ya mwelekeo wa kuingia katika Krismass wakiwa vinara lakini huwenda wakahukumiwa na historia ya ligi hiyo ya Premier mwishoni mwa juma hili.
Tujikumbushe historia ya kumaliza katika usukani wa msimamo wa ligi kuu ya England wakati kama huu na matokeo ya mwisho wa msimu yalivyokuwa huko nyuma
Festive leaders Year Finished
Norwich City..............................1993 3
Manchester United....................1994 1
Blackburn Rovers......................1995 1
Newcastle United.......................1996 2
Liverpool...................................1997 4
Manchester United....................1998 2
Aston Villa.................................1999 6
Leeds United.............................2000 3
Manchester United....................2001 1
Newcastle United.......................2002 4
Arsenal......................................2003 2
Manchester United....................2004 3
Chelsea.....................................2005 1
Chelsea.....................................2006 1
Manchester United.....................2007 1
Arsenal......................................2008 3
Liverpool....................................2009 2
Chelsea.....................................2010 1
Manchester United.....................2011 1
Manchester City.........................2012 1
Manchester United.....................2013 1

Katika ukweli wake ni kwamba hiyo haikupi uhakika wa kumaliza kwa mafanikio lakini inatia moyo na kujitahidi kupigana kwa kujiweka vizuri zaidi ambapo ukitazama huko nyuma kuwa vilabu saba kati ya vinane vilivyo maliza msimu wa Krismas wakiwa vinara wa msimamo walifanikiwa kuwa mabingwa wa Premier League.
Arsenal
inaweza kusalia katika usukani endapo itashinda dhidi ya Chelsea katika mchezo mgumu utakao pigwa
Emirates Jumatatu jioni lakini inapaswa pia kutambua kuwa wengine wanaweza kupata nafasi hiyo maarufu kama 'Christmas No 1'.
Liverpool,
ambao wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 14 katika michezo yao mitatu ya ligi wanaweza kuwapiku Arsenal endapo tu watafanikiwa kuwafunga Cardiff katika dimba la Anfield Jumamosi na wakijivunia faida ya magoli ya kufunga na kufungwa endapo Arsenal wakifungwa na Chelsea.
Kwa upande wa kikosi cha kocha Mreno Jose Mourinho watafanikiwa kutinga kileleni mwa msimamo na kufurahia msimu wa sikukuu endapo watashinda mchezo wao wa uwanja wa Emirates na endapo Liverpool wakishindwa kuwafunga Cardiff Jumamosi.
Bado ni alama nne tu zinazo itenganisha Arsenal iliyo kileleni na Everton walio katika nafasi ya tano ambapo kwao mbio za kuwania taji huwa hazishindikani kwao.

Takwimu zimekuwa zikiipendelea Manchester United katika kipindi kama hiki, ambao wamekuwa si zaidi ya nafasi ya sita katika Krismass na swali lingine ni endapo Tottenham au Newcastle watashinda michezo yao.

Sir Alex Ferguson akinyanyua kombe la ligi kuu mwezi May

Kwanini ni ngumu kugonga glass wakati kama huu ukiwa chini ya msimamo wa ligi.
Soma Jedwali chini kujua walio ingia katika msimu wa sikukuu za Krismass wakishika mkia miaka kumi iliyopita.
Team Season Points Pos Final Pts Finish Relegated?
No comments:
Post a Comment