Mshambuliaji Luis Suarez leo ameendelea kuonyesha kiwango chake katika msimu huu na kuweka Liverpool kileleni mwa ligi kuu ya England na kukifanya kibarua cha meneja wa Cardiff Malky Mackay kuwa katika wakati mgumu.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay ambaye aliwashangaza watu hapo jana kwa kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu yake amefikisha jumla ya mabao 19 msimu akichagiza ushindi wa timu wa mabao 3-1 dhidi ya Cardiff.
Raheem
Sterling pia ameiingia katika orodha ya wafungaji akifunga bao la pili licha ya kwamba Jordon alifunga bao la kufuatia machozi la Cardiff kunako dakika ya 58.
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez akishangilia bao katika mchezo dhidi ya Cardiff uliopigwa
Matokeo hayo ya mchezo yanamuweka Mackay katika hali tete zaidi kwani tayari alikwisha kuwekwa katika tahadhari na Vincent Tan. Mmiliki huyo wa klabu hiyo alikuwepo hii leo Anfield kushuhudia mpaka mapumziko mambo kuwa magumu kwani tayari Liverpool walikuwa wamesha kamilisha karamu yao ya magoli.
Ni mpaka lini Mackay atasalia ndani ya klabu hiyo hilo ni swali linalosubiri majibu masaa machache yajayo.
Wakitiwa mafuta na magoli ya Suarez sasa Liverpool imewapiku walikokuwa vinara kwa muda mrefu Arsenal, ambao wanatarajiwakukutana dhidi ya Chelsea Jumatatu wakati msimu ukiwa unakaribia kufikia katikati na Liverpool wakionekana kama wapinzani wakubwa wa taji msimu huu wakikimbizana vilivyo na Gunners, Manchester City na Chelsea.
Suarez sasa amefikisha jumla ya magoli 19 katika jumla ya michezo 12 aliyocheza akifunga magoli 10 katika michezo minne ya mwisho.
No comments:
Post a Comment