KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 21, 2013

Massimilian Allegri hana shaka na kikosi cha AC Milan

 Massimilian Allegri hana shaka na kikosi cha AC Milan wakati huu ambapo wanajiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya wapinzani wao wakubwa katika soka la Italia Inter Milan.
Rossoneri ilimsajili  Adil Rami kwa mkopo akitokea Valencia kabla ya mwezi Januari na Keisuke Honda akitokea CSKA Moscow, lakini kocha huyo wa San haonyeshi nia ya kuongeza mchezaji akisema kikosi chake kimeshiba.
"Tunapaswa kupunguza ukubwa wa kikosi na nitaongea na utawala juu ya hilo. Kikosi chetu kinajumuisha wachezaji 24 mpaka 25.
"sitaki kuzungumzia juu ya mtu aliyeripotiwa kutakiwa na Milan  Radja Nainggolan kwasababu ni mchezaji wa Cagliari na sitaki kumsumbua.
"tumezungumza mengi kuhusu uhamisho lakini utawala utafuatialia. Rami na Honda ni usajili.