KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 19, 2013

OKWI AWASILI RASMI YANGA

Moses Katabaro na Seif Ahmed wakimpokea Okwi
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Emmanuel Okwi amewasili leo mchana majira ya saa 9:45 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyererer akitokea nchini Uganda kwa shirika la ndege la Rwanda Air.

Okwi amekuja kujiunga na timu yake mpya Yanga SC ambayo ataanza kuitumikia katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya Kimataifa.
 
Mara baada ya kuwasili JK Nyerere Okwi alipokelewa na vipngozi wa kamati ya mashindano sambamba na washabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla.
 
Okwi akiongea na waandishi wa habari uwanja wa ndege amesema anashukuru kwa kufika salama jijini Dar es Salaam na hasa katika timu yake mpya ya Yanga.
 
Kikubwa ameahidi kucheza kwa uwezo wake wote kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri katika mashindano yote.
 
Okwi mara baada ya kuwasalimia washabiki na wanachama wa Yanga uwanja wa Kaunda moja kwa moja ameungana na wachezaji wenzake katika kambi iliyopo Protea kujiandaa na mchezo wa jumapili.

No comments:

Post a Comment