Ukisikiliza clip hiyo hapo juu Emmanuel Okwi akiongea baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu Etoile du Sahel ya Tunisia akitokea Simba SC ya Tanzania utaona ni namna gani mchezaji huyo alivyoshindwa kuheshimu kauli zake kwa vitendo.
Alichotamka hapo juu mbele ya kamera ya mwandishi wa habari wa klabu hiyo ni kuwa hatua ya yeye kujiunga na klabu hiyo kigogo nchini Tunisia na barani Afrika kwa ujumla ni kubwa sana akitokea Tanzania na kwamba hiyo ni hatua nyingine kwake ya kusonga mbele na kucheza soka Ulaya na kurudi nyuma.
Nimesikitishwa na Okwi mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kurejea Tanzania kwa mara nyingine tena na kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu kwa wapinzani wakubwa wa klabu yake ya zamani Yanga Afrika.
Sina maslahi na klabu yoyote kati hizo mbili za Simba na Yanga isipokuwa kauli hiyo na maamuzi yake ni vitu viwili tofauti sana nina mashaka kuwa soka yake inaelekea kuishia katika fitna za Soka la Afrika mashariki na kati.
Mshambuliaji huyu raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na Simba mwaka 2010 akitokea SC Villa ya Uganda ambapo taarifa zilieleza kuwa aliuzwa kwa ada ya dolari za kimarekani $300,00 na yeye atakuwa akipokea dolari $15,000 kwa mwezi.
Kubwa kuliko ni kuwa katika makubaliano ya Simba kumuuza Okwi kwenda kwa Etoile du Sahel ni kwamba endapo klabu hiyo ya nchini Tunisia itamuuza kwenda klabu nyingine, ni kuwa Simba itapokea asilimia 10 ya mauzo yake sasa hilo ni wazi kuwa Simba imekula kwao.
No comments:
Post a Comment