KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 19, 2013

Wilshere agoma kusimama michezo miwili kwa kuonyesha dole la kati kwa mashabiki wa City.

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere amekubaliana na adhabu ya chama cha soka nchini England FA kufuatia dhihaka ya kidole cha kati kwa mashabiki wa Manchester City, lakini amepinga adhabu hiyo kwa upande mwingine kwa kusimama michezo miwili ambapo shauri dhidi yake litasikilizwa baadaye hii leo Alhamisi na kamati ya nidhamu.

Chama cha soka cha England kilipitia taarifa ya mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson kabla ya kusikiliza kesi dhidi ya Wilshere kufuatia picha za televisheni kumuonyesha akiinua kidole cha kati kuelekea kwa mashabiki wa timu mwenyeji.

Meneja wa Arsenal  Arsene Wenger hapo kabla alikaririwa akisema klabu yake itakubaliana na adhabu hiyo ya FA kwa kiungo wake.

No comments:

Post a Comment