Wakati msimu wa sherehe za Krismass na mwaka mpya ukiwa unazidi kushika kasi huku mameneja wa vilabu vya England (Premier League) wakikosa usingizi kwa hofu ya nini kitatokea kesho huko Hispania Real Madrid iliwakutanisha pamoja nyota wao wa vikosi vya timu za mpira wa miguu na kikapu ambao waliokuwa katika mitindo mbalimbali ya kisasa.
Hakukuwa na mavazi ya ajabu ajabu yaliyoonekana ambapo wachezaji walikuwa huru kunywa na wakifurahia milo huku wachezaji wa vikosi vyote wa Real
Madrid wakikusanyika kwa pamoja wakisheherekea mchana wa jana.
Wazo la kuzindua sherehe za Krismass na mwaka mpya kwa mtindo wa chakula cha mchana hapo jana Jumatatu linaonekana ni jambo la kawaida kwa Waingereza ambapo Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos
na Gareth Bale walijumuika na wenzao wenye uzoefu ambao si wazoefu sana na mambo hayo ndani ya Bernabeu.


Cristiano Ronaldo (kulia) akiwa na mcheza kikapu nyota wa Real Madrid Marcus Slaughter wakiwa wamezungukwa na glasi za vinywaji

Gareth Bale (kulia) akitaniana na Mbrazil Marcelo

Rais Florentino Perez (katikati) akizungumza na wachezaji Marcelo na Gareth Bale
Nyota wa Los Blancos waliuungana na wachezaji klabu hiyo wa mchezo kikapu ikiwa ni pamoja na Marcus Slaughter na Dontaye Draper.
Kituko ni pale Balozi wa klabu hiyo Zinedine Zidane alionekana mdogo alipojipima urefu na wachezaji wa kikapu Salah Mejri na Ioannis Bourousis ambao timu yao ya kikapu msimu uliopita walifika fainali ya ligi ya mabingwa ya kikapu wakifungwa katika fainali na Olympiakos.

Zinedine Zidane (katikati) akionekana mdogo kwa urefu ukilinganisha na wachezaji kikapu wa Real Madrid Salah Mejri (kushoto) na Ioannis Bourousis


President Florentino Perez akiongea na Raphael Varane (kushoto) na Alvaro Arbeloa (kulia)

Wachezaji wa timu zote mbili za Real Madrid za kikapu na mpira wa miguu wakiwa wamehudhuria sherehe za uzinduzi wa msimu wa krismas kwa timu yao ambazo zilifanyika jana Jumatatu Estadio
Santiago Bernabeu
No comments:
Post a Comment