KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 9, 2013

Shabiki wa Manchester nchini Kenya ajiua kwa kichapo cha Newcastle mwishoni mwa juma.

Shabiki wa Manchester United amejiua jijini Nairobi kufuatia matokeo ya timu yake kufungwa bao 1-0 na Newcastle United mwishoni mwa juma, polisi imethibtisha.
John Macharia ameripotiwa kujitupa kutoka ghorofani katika nyumba moja maarufu yenye maduka katikati ya jiji la Nairobi baada ya mchezo huo uliopigwa Old Trafford Jumamosi.

Kamanda wa poli jijini humo Benson Kibui ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa
‘Macharia alijirusha kutoka ghorofa ya saba katika nyumba ya Pipeline Estate baada ya kushuhudia timu yake ikibamizwa na bao 1-0 na Newcastle na hivyo kuamua kujiua.
Polisi huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wakenya kuziunga mkono timu zao za Kenya kuliko timu za kigeni hususani barani Uropa.

‘The football fans should enjoy the matches… but they should not commit suicide since life is very precious,’

Kichapo cha Manchester United mwishoni mwa juma kimeiacha United alama 13 nyuma ya vinara Arsenal .

No comments:

Post a Comment