Waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi Azam FC ya jijini Dar es Salam leo wameyaaga mashindno hayo baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka KCC ya Uganda mchezo wa nusu fainali ya kwanza ilipigwa katika uwanja wa Amani mjini Unguja.
Bao la ushindi la KCC limefungwa katika dakika mwisho za mchezo na William Wadri
akiunganisha krosi ya
Habib Kavuma.
Mpaka kufikia dakika ya 51 ya mchezo Azam walikuwa mbele kwa mabao 2-1 kabla ya Tony Odur kuandika bao la kusawazisha lkufuatia mpira wa Krosi wa Habib Kavuma.
Hadi
mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa mabao 2-1, yaliyotiwa
kimiani na Joseph Lubasha Kimwaga yote dakika za 16 na 32 akifunga bao la
kwanza kwa kichwa akiunganisha kona iliyochongwa na beki wa kulia Erasto
Nyoni kutoka wingi ya kulia.
Bao
la pili Kamwaga aliitokea krosi ya chini ya mshambuliaji hatari wa
Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche kutoka kushoto na kuteleza nayo hadi
nyavuni.
Baada
ya kupata bao hilo, Azam walionekana kutaka kuwadharau wapinzani wao,
walioitumia vyema fursa hiyo kupata bao moja kabla ya mapumziko,
lililofungwa na Ibrahim Kiiza dakika ya 37.
Kipindi
cha pili, mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcameroon, Joseph Marius
Omog kuwatoa wachezaji wote wa safu ya mbele Kipre Tchetche, Joseph
Kimwaga na Brian Umony na kuwaingiza Muamad Ismail Kone, Ibrahim
Mwaipopo na Farid Mussa yaliigharimu timu.
Wachezaji
wote walioingia walishindwa kucheza vizuri kama waliotoka na ndipo KCC
ilipoutumia mwanya huo kutoka nyuma na kushinda mechi.
Baadaye kutakuwa na mchezo wa nusu fainali ya pili baina ya Simba SC
ya Dar es Salaam na URA ya Uganda.
Mchezaji Joseph Kimwaga alikabidhiwa king’amuzi na rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi baada ya kutajwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment