KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 3, 2014

Paul Pogba akumbuka usia wa Furguson juu ya ubaguzi, lakini pia azungumzia ndoto za kujiunga na Arsenal na Barcelona.

 Kiungo wa Juventus ya Italia Paul Pogba ametanabaisha kuwa ilikuwa ni ndoto kwake ya kuchezea vilabu viwili vikubwa Ulaya vya Barcelona na Arsenal na kuongeza kuwa pamoja na hayo bado anajisikia vizuri akiwa ndani ya klabu yake ya sasa.

Nyota huyo wa kimataifa w Ufarasna alijiunga na Bianconeri akitokea Manchester United kiangazi 2012 na tangu wakati huo amekuwa mchezaji muhimu katika klabu yake hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A na wakiwa watetezi wa taji la ligi hiyo.

Amekuwa akihusishwa sana na kutaka kuelekea katika vilabu vikubwa hususani Paris Saint-Germain, ambapo kigogo hicho kingine cha Ufaransa mapema wiki hii wakikaririwa wakisema kuwa wanataka kumsajili Pogba mwishoni mwa msimu, lakini anaonekana ni mwenye furaha zaidi kuendelea kuwepo katika kikosi cha meneja Antonio Conte.

"Najisikia vizuri sana hapa Juventus, licha ya kwamba siwezi kukanusha kuwa nimekuwa na ndoto ya kuchezea ama Arsenal au Barcelona wakati nilipokuwa mtoto" Amekaririwa Pogba mwenye umri wa miaka 20 na gazeti la, La Repubblica.

"kwangu, Juventus ni wakati ule wa Zinedine Zidane, David Trezeguet na Pavel Nedved. walikuwa na vipaji, viwango, nidhamu na waliungana kama timu"

Pogba akaendelea kwa kuzungumzia maamuzi yake ya kuihama Manchester United na kuelekea Juve akisema Sir Alex Ferguson alimshauri asijiunge na kigogo hicho cha Turin kwani kuna ubaguzi wa rangi.

"Namuheshimu sana Ferguson. aliniamini licha ya kwamba sikucheza sana. Aliniambia nisiende Italia. Alinionya dhidi ya ubaguzi wa Italia na alidhani sitajisikia vizuri hapa.

"Kuhusu ubaguzi, hakuna taifa lenye kinga dhidi ya ubaguzi. Pia hata England upo pia. Angalia kilichotokea kwa John Terry na Luis Suarez."

No comments:

Post a Comment