KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 3, 2014

Masikini mzee Wenger sasa ameanza kuota ndoto za ubingwa baada ya muongo mzima kupita

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameendelea kusisitiza kuwa vijana wake wameonesha ushahidi tosha kuwa wana nguvu na ari inayohitajika kunyakua taji la Ligi ya Premier ya Uingereza msimu huu baada ya kungoja kwa muda mrefu.

Ushindi wao wa bao 2-0 wa dakika za mwisho mwisho dhidi ya Cardiff City Jumatano, umempa matumaini makubwa mzee Wenger ya kuwa Arsenal ni miongoni mwa wale wanaogombania kikombe cha ubingwa walikishinda mara ya mwisho mwongo mmoja uliopita. 

Ingawa Manchester City na Chelsea wanamfuata katika msimamo wa ligi hiyo Arsenal wanazidi kuwapinga kujitutumua msimu huu na wakitaka wababe hao wasalimu amri. 

Nicklas Bendtner na Theo Walcott walikamilisha ushindi huo ikisalia dakika chache kipenga cha mwisho kupulizwa na kuipa  Arsenal uongozi wa msimamo. 

“Kuna umoja dhabi kikosini. Wachezaji wananidhamu na hilo linaleta tofauti. Ikiwa hilo halipo mashindanoni, basi hauna nafasi ya kutwaa ubingwa,” Wenger alisema.

Bendtner aliibuka shujaa kwenye mechi hiyo baada ya kufunga la kwanza ikisalia dakika mbili baada ya Cardiff kumudu mashabulizi ya Arsenal kwa kujenga mwamba kwenye ngome yao. 

Raia huyo wa Denmark anazidi kuwashawishi wale ambao walikuwa wamekata tamaa na uwezo wake wakati fulani, huku akiwakera mashabiki wa Arsenal. 

“Ni mchezaji ambaye amepitia mengi magumu kwa hivyo, ningelitaka kumsifu sana,” anasema Wenger, ambaye alitangaza kwamba mshambuliaji huyu aliumiza kifundo cha mguu wakati akifunga bao lake.

“Nilimwambia kuwa amefikia kiwango nilichotaka awe na akiendelea kunawiri kwa njia hiyo, atarejea kwenye kikosi.

“Kwa bahati mbaya, alijeruhiwa na inaonekana atakosa mchezo wiki kadhaa. Nina huzuni sana hususan kwake binafsi na timu yote kwa ujumla.”

No comments:

Post a Comment