Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara na vinara wa ligi hiyo
timu ya Young Africans itashuka dimbani siku ya jumatano kucheza mchezo
wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Altay S.K iliyopo Ligi
Daraja la Pli nchini Uturuki.
Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi leo asubuhi na jioni
katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side kujiandaa na mchezo huo
wa siku ya jumatao ambao ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Kaimu
kocha mkuu Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wote
wanaendelea vizuri katika kambi ya mafunzo, hakuna mchezaji ambaye
amekosa mazoezi hata siku moja na hali ya hewa inaruhusu kabisa kufanya
mazoezi hivyo vijana wanaitumia ipasavyo nafasi hiyo.
Akiongelea
mchezo wa keshokutwa Mkwasa amesema anawaandaa vijana kuendelea kufanya
vizuri katika mchezo huona ataendelea kutoa nafasi kwa kila mchezaji
aliyekuja nchini Uturuki apate nafasi ya kucheza kwani kupata nafasi ya
kucheza michezo ya kirafiki huku ni njia ya kuwakomaza na kuweza
kujiamani katika michezo ya kimataifa.
Kesho timu ya Young
Africans itafanya mazoezi mara moja tu asubuhi kujiandaa na mchezo huo
wa jumatano dhidi ya timu ya Altay SK ambayo pia inajiandaa na mzunguko
wa pili wa Ligi Daraja Pili nchini Uturuki.
Mara baada ya mchezo
huo wa jumatano Young Africans itakamlisha ziara yake ya mafunzo wiki
ijayo kwa kucheza na timu ya Simurq Zaqatala FC ya nchini Azberbaijan
iliyopo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo na msimu uliopita ikiwa imekamata
nafasi ya nne kwenye msimamo wa Azerbaijan Premier League.
No comments:
Post a Comment