Fifa imeshangazwa na kelele za ukosoaji za meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini dhidi ya mwamuzi Jonas Eriksson na kuziita kuwa ni upuuzi.
Bosi huyo wa Man City alizungumzia uwezo wa mwamuzi Eriksson usiku wa jana katika mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Barcelona kuwa hakuweza kuchezesha vema na kwamba mwamuzi huyo raia wa Sweden ndiye aliyekuwa chagizo la kufungwa kwao.
Kelele hizo zimejibiwa na makamu wa Rais wa Fifa na bosi wa waamuzi Jim Boyce akisema
‘It
is absolute nonsense to say a referee should not be chosen for an
important match because he comes from a smaller country.
‘If the referee has proved himself at the top level it should not matter what country they come from.
‘All the referees who have been chosen for the World Cup have been
assessed by experienced officials who have been involved at Fifa and
Uefa level and marked on their performances in the World Cup and
confederation competitions at a high level.’
Eriksson mwenye umri wa miaka 39, amechaguliwa kuchezesha michezo ya kombe la dunia nchini Brazil na Boyce ameongeza kuwa
‘Nimeangalia maoni ya meneja na kuhusisha na mchezo na nimeuona mchezo mimi mwenyewe na kwa maoni yangu ni kuwa mwamuzi alikuwa na wakati mzuri. Ana uzoefu mkubwa na amechaguliwa kuchezesha kombe la dunia kwasababu ya ripoti yake nzuri katika michuano ya Ulaya’
Eriksson alitoa pigo la zawadi kunako dakika ya 54 kufuatia Martin Demichellis kumfanyia madhambi Lionel Messi katika kisanduku cha hatari.
No comments:
Post a Comment