KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, February 24, 2014

Michezo ya Olympiki 2014 yafungwa rasmi jana Russian fed ikikomba medali nyingi zaidi

Michezo ya majira ya baridi ya Olympics ilifikia mwisho jana Jumapili ambapo wenyeji Urusi imejinyakulia medali nyingi zaidi na Canada ikanyakua taji la mpira ya magongo katika barafu kwa wanaume, lakini taarifa kwamba wachezaji wawili zaidi wamegundulika kutumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu misuli zimeleta hali ya kufifia kwa mwanga wa mashindano hayo.
Canada ilijinyakulia ubingwa wa mpira wa magongo kwa kuiangusha Sweden kwa mabao 3-0 na kutetea ubingwa wao huo kwa wanaume, lakini ushindi mara mbili kwa Urusi umeihakikishia nchi hiyo kupata medali 13 za dhahabu dhidi ya 11 za Norway.
Madhila ya Sweden yaliongezwa na taarifa kuwa mshambuliaji wao Nicklas Backstrom amegundilika kuwa anatumia madawa ya kuongeza nguvu misuli , Doping.

 Maafisa wa timu hiyo wameilalamikia kamati ya kimataifa ya Olimpiki  IOC, kwasababu walifahamishwa saa mbili tu kabla ya michezo hiyo kuanza. Hata hivyo rais wa IOC Thomas Bach amesema kuwa wenyeji Urusi wamedhihirisha kuwa wakosoaji wao hawakuwa sahihi.
Kwa upande wa kikosi cha Ujerumani katika michezo hiyo mambo hayakuwa kama yalivyotarajiwa. Hali ya mambo anasema kiongozi wa kikosi hicho Michael Vesper haikuwa nzuri.
"Lengo letu halikutimia. Tumekuwa na matokeo mazuri kabisa katika wiki moja na nusu ya mwanzo, ambapo tulionesha ubora wetu kwa mataifa. Na baada ya hapo mambo hayakwenda vizuri."

Hadi wakati huo wa kuporomoka , Evi Sachenbacher-Stehle mchezaji wa mbio za kwenye barafu na kulenga shabaha, alionekana tu kwamba madawa hayo yalionekana kuwa ni virutubisho katika chakula. Na kamati ya kimataifa ya olimpiki ilikubali matokeo ya mchezaji huyo katika michezo ya Sochi. Lakini siku ya Jumamosi mchezaji huyo alibidi kuondolewa kutoka katika kikosi cha Ujerumani. Waziri wa sheria wa Ujerumani Heiko Maas akizungumzia kuhusu hali hiyo amesema.
"Tunataka , kwamba hapo katika siku za usoni yeyoyte ambaye atapatikana na hatia kama hiyo ya doping, ama hata yeyote ambaye atapatikana na madawa kama hayo na pia kuuza , ataadhibiwa. Na kufungwa hadi miaka mitano jela."
Hiyo ndio hali iliyokuwa katika kambi ya kikosi cha timu ya Ujerumani katika olimpiki ya majira ya baridi ya mjini Sochi. Na hadi hapo ndio sina budi kusema tumefikia mwisho wa kuwaletea habari hizi za michezo kwa leo jina langu ni Sekione Kitojo, hadi mara nyingine kwaherini.
 Medal count
Rank Country Gold Silver Bronze Total
1 Russian Fed. 13 11 9 33
2 Norway 11 5 10 26
3 Canada 10 10 5 25
4 United States 9 7 12 28
5 Netherlands 8 7 9 24
6 Germany 8 6 5 19
7 Switzerland 6 3 2 11
8 Belarus 5 0 1 6
9 Austria 4 8 5 17
10 France 4 4 7 15
11 Poland 4 1 1 6
12 China 3 4 2 9
13 Korea 3 3 2 8
14 Sweden 2 7 6 15
15 Czech Republic 2 4 2 8
16 Slovenia 2 2 4 8
17 Japan 1 4 3 8
18 Finland 1 3 1 5
19 Great Britain 1 1 2 4
20 Ukraine 1 0 1 2
21 Slovakia 1 0 0 1
22 Italy 0 2 6 8
23 Latvia 0 2 2 4
24 Australia 0 2 1 3
25 Croatia 0 1 0 1
26 Kazakhstan 0 0 1 1
- Albania 0 0 0 0
- Andorra 0 0 0 0
- Argentina 0 0 0 0
- Armenia 0 0 0 0
- Azerbaijan 0 0 0 0
- Belgium 0 0 0 0
- Bermuda 0 0 0 0
- Bosnia and Herzegovina 0 0 0 0
- Brazil 0 0 0 0
- Bulgaria 0 0 0 0
- Cayman Islands 0 0 0 0
- Chile 0 0 0 0
- Chinese Taipei 0 0 0 0
- Cyprus 0 0 0 0
- Denmark 0 0 0 0
- Dominica 0 0 0 0
- Estonia 0 0 0 0
- Georgia 0 0 0 0
- Greece 0 0 0 0
- Hong Kong, CHN 0 0 0 0
- Hungary 0 0 0 0
- Iceland 0 0 0 0
- Independent Olympic Participant 0 0 0 0
- India 0 0 0 0
- IR Iran 0 0 0 0
- Ireland 0 0 0 0
- Israel 0 0 0 0
- Jamaica 0 0 0 0
- Kyrgyzstan 0 0 0 0
- Lebanon 0 0 0 0
- Liechtenstein 0 0 0 0
- Lithuania 0 0 0 0
- Luxembourg 0 0 0 0
- Malta 0 0 0 0
- Mexico 0 0 0 0
- Monaco 0 0 0 0
- Mongolia 0 0 0 0
- Montenegro 0 0 0 0
- Morocco 0 0 0 0
- Nepal 0 0 0 0
- New Zealand 0 0 0 0
- Pakistan 0 0 0 0
- Paraguay 0 0 0 0
- Peru 0 0 0 0
- Philippines 0 0 0 0
- Portugal 0 0 0 0
- Rep. of Moldova 0 0 0 0
- Romania 0 0 0 0
- San Marino 0 0 0 0
- Serbia 0 0 0 0
- Spain 0 0 0 0
- Tajikistan 0 0 0 0
- Thailand 0 0 0 0
- The Former Yugoslav Republic of Macedonia 0 0 0 0
- Timor-Leste 0 0 0 0
- Togo 0 0 0 0
- Tonga 0 0 0 0
- Turkey 0 0 0 0
- Uzbekistan 0 0 0 0
- Venezuela 0 0 0 0
- Virgin Isl, B 0 0 0 0
- Virgin Isl, US 0 0 0 0
- Zimbabwe 0 0 0 0

No comments:

Post a Comment