KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, February 2, 2014

Mshindano ya wazi ya ngumi" Mkoa wa Kigoma wawasili na mabondia 10

KOCHA wa timu ya ngumi  ya Mkoa wa Kigoma Juma Lesso amesema timu yake ya mkoa imekuja kamili kwa ajili ya mashindano ya wazi yatakayofanyika Feb 5
katika viwanja vya Tanganyika Peckers vilivyopo kawe jijini Dar es salaam

Hii mara ya kwanza kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kushiriki mashindano makubwa kama haya na timu hiyo ambayo imeweka kambi yake maeneo ya kawe kabla ya hapo ilikuwa maeneo ya mabibo na sasa kawe kwani mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Feb mosi mwaka huu na sasa yakisogezwa mbele hadi  feb 5

Amekaririwa akisema
"Tunamshukulu sana Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya kwa kuhakikisha tunashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza"
 
Timu hiyo ambayo imekuja na wachezaji kumi kati ya hao wanawake watatu na wanaume saba ambao wakekuja kuwakilisha mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuchukuwa ubingwa huo ambao upo wazi

Lesso ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo huo ambaye amepitia kozi ya kimataifa ya mchezo aliwataja baadhi ya mabondia aliokuja nao kuwa ni Agnes Mushi, Eliza Josefu, Rashidi na Abasi na wengine ambao walikuwa katika kambi ya mkoa huu  wa Kigoma 

No comments:

Post a Comment