Olivier Giroud amerejea kwa mbwembwe hii leo katika kikosi cha Arsenal kwa kufunga goli murua dhidi ya Sunderland huku sasa akijaribi kukisahau kipindi cha wiki ngumu iliyopita.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufarasna hakuanza katika michezo miwili iliyopita ya timu yake ambapo alitakiwa kumuomba radhi mkewe kutoka na kashfa ya kufanya ufuska na mwanamitindo mmoja.
Giroud alitupia ujumbe katika mtandao wa Twitter kuwa atafanya kila awezalo kurudisha upya mapenzi na heshima yake kwa mkewe Jennifer, ambapo kashfa hiyo ilionekana kumvuruga kiasi kutoswa katika kikosi kabla ya kurejeshwa upya katika mchezo dhidi ya Sunderland na leo akianza kuandika bao la kwanza.

Ikiwa ni kama kujaribu kurejesha penzi upya kwa mkewe hii alishangilia goli hilo kwa kuonyesha kidole kilichokuwa na pete ya ndoa na kuibusu pete hiyo kabla ya kuwapigia saluti mashabiki wa Arsenal.
No comments:
Post a Comment