KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 19, 2014

Arsene Wenger kuongeza kandarasi Emirate mwishoni mwa wiki

 Arsene Wenger atamaliza minong'ono ya muda mrefu inayohusu mkataba wake mwishoni mwa wiki hii kwa kuingia kandarasi nyingine.

Wenger, ambaye anakaribia kukamilisha umri wa miaka 65 mwezi Oktoba, anaelekea kuanguka saini na kumalizia kile ninachoonekana kama ni kumalizia mkataba wa mwisho kabla ya kustaafu.

Arsenal na Wenger wanatazamiwa kuingia makubaliano ya malipo ya pauni milioni £7.5 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wenger, ambaye atakabidhiwa fungu nene la usajili wa kiangazi katika historia ya uhamisho wa wachezaji wa klabu hiyo, ameamua kuendelea kusalia  baada ya kufikia malengo aliyojiwekea ya kushinda FA Cup na kumaliza katika nafasi nne za juu katika 'Premier League'.