Manchester United imemtangaza rasmi Louis van Gaal kuwa meneja wao mpya kufuatia kumfuta kazi David Moyes mwezi uliopita.
Taarifa zimethibitisha kuwa Mduchi huyo atakuwa anachukua nafasi ya bosi wa muda Ryan Giggs aliyechukua kiti hicho kilichokuwa cha moto kuelekea mwishoni mwa msimu. Giggs raia wa Wells ameteuliwa kuwa meneja msaidizi.
Frans
Hoek na Marcel Bout wanaungana kuwa makocha wasaidizi huku Van Gaal ambaye ni meneja wa sasa wa timu ya taifa ya Uholanzi akitarajiwa kuanza kazi yake mpya baada ya fainali ya kombe la dunia la Kiangazi nchini Brazil.
Mwanga mpya: Louis van Gaal, akiwa katika picha na mshambuliaji wake wa baadaye Robin van Persie, ambaye kwasasa yuko naye katika kikosi cha Uholanzi.
Van Gaal atakuwa akikifundisha kikosi cha Uholanzi kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia
Taarifa ya Manchester United imesomeka
'Louis van Gaal atachukua nafasi ya umeneja kuanzia msimu wa 2014/15 . Amesaini mkataba wa miaka mitatu.
'Louis mwenye umri wa miaka 62 amekuwa akifundisha katika kiwango cha juu barani Ulaya kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 na katika kipindi hicho ameshinda ameshinda mataji ya ndani na vikapu vya ndani katika nchi tatu pamoja na kushinda taji la vilabu Ulaya (UEFA Champions League), UEFA Cup,Intercontinental Cup, na mataji mawili ya Ulaya ya UEFA Super Cups ikiwa ni pamoja na vikombe vya ndani ya Super Cups katika nchi za Uholanzi na Ujerumani.
'Atachukua nafasi yake baada ya kombe la dunia la FIFA ambako atakuwa akikiongoza kikosi cha Uholanzi.
Ryan Giggs, mchezaji mwenye sifa isiyokifani katika 'English football' na ambaye ni mchezaji mwenye rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi ndani ya United ameteuliwa kuwa meneja msaidizi. Ryan alikuwa kazini kwa muda katika michezo minne ya ligi msimu uliomalizika 2013/14 '
Ryan Giggs, mchezaji mwenye sifa isiyokifani katika 'English football' na ambaye ni mchezaji mwenye rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi ndani ya United ameteuliwa kuwa meneja msaidizi. Ryan alikuwa kazini kwa muda katika michezo minne ya ligi msimu uliomalizika 2013/14 '
Akitangaza uteuzi huo, Ed Woodward amesema
'In Louis van Gaal, tumemtaka mtu mwenye rekodi iliyotukuka katika mchezo huu mpaka sasa. Van Gaal ana mengi katika fani hii mpaka kufikia sasa na Old Trafford inampa nafasi ya kuzuba pengo hilo akiandika historia mpya ndani ya Manchester United'
Meneja huyo wa zamani wa Barcelona hakuwahi kuwa meneja wa klabu yoyote nchini England lakini amekuwa na uzoefu mikubwa alioupata akiwa na vilabu kadhaa barani Ulaya vikiwemo Ajax, AZ Alkmaar na Bayern Munich, ikiwa ni pamoja na kuwa kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi.
Wamiliki wa United
kundi maarufu la 'Glazer family' linajiandaa kumpa msaada mkubwa meneja mpya katika kipindi cha usajili wa wachezaji ambapo mapendekezo yake yakiwagusa nyota kadhaa kama Mats Hummels, Marco Reus na Toni Kroos.
LOUIS VAN GAAL FACTFILE
Born: August 8, 1951
Age: 62
Place of birth: Amsterdam, Holland
Clubs played for: Ajax, Royal Antwerp, Telstar, Sparta Rotterdam, AZ Alkmaar
Total appearances: 333
Total goals: 34
Clubs managed: Ajax, Barcelona (two spells), AZ Alkmaar, Bayern Munich
Countries managed: Holland (2000-02 and 2012-present)
Honours as a manager: Eredivisie (1993-94, 1994-95, 1995-96, 2008-09), UEFA Cup 1991-92, Champions League 1994-95, UEFA Super Cup (1995 and 1997), La Liga (1997-98 and 1998-99), Copa del Rey (1997-98), Bundesliga 2009-10
Van Gaal ametaka kuungana na kocha wa makipa Frans Hoek(pichani juu)kuungana naye kuchukua nafasi ya Chris Woods
No comments:
Post a Comment