Barcelona wameanza kumkodolea macho Eden Hazard kwa kuchungulia hali ya mambo ndani ya daraja la Stamford hizi zikiwa ni taarifa ambazo zimeanza kuzagaa nchini Hispania.
Winga huyo raia wa Belgiam aliachwa katika kikosi cha kwanza cha timu ya Chelsea kilicho kwenda suluhu na Norwich, huku Jose Mourinho akidai kuwa mchezaji huyo hakujitoa katika timu wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico.
Meneja Mourinho alitoa maoni baada ya mchezo dhidi ya Atletico Madrid, akidai Hazard alikosoa mbinu za klabu licha ya kuwa ni sehemu ya waliosababisha kufungwa kwa magoli mawili katika kichapo cha mabao 3-1.
Gazeti la El Mundo Deportivo limedai kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuuzwa na Chelsea kiangazi licha ya kuwa mchezaji wao bora wa msimu na tayari vilabu vya Barca, Real Madrid na Paris Saint Germain wanaonekana kusubiri mkono udondoke na kuanza kunyang'anyana kama fisi.
No comments:
Post a Comment