Mtaalamu wa FIFA akagua uwanja wa Kaitaba
|
Dr. Ian McClements akichimba chini ili kupima na kuona aina ya udongo ulio
chini katika uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba kabla ya mradi wa uwekaji nyasi bandia kuanza.
Uwanja wa Kaitaba na Nyamagana jijini Mwanza vinatarajiwa kuwekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa shirikisho la soka dunia FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa
Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal
Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar
es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
|
No comments:
Post a Comment