Jabir Azizi Stima anayecheka |
KLabu ya Azam FC hii leo imetangaza kutokuongeza mikataba ya wachezaji wao saba huku ikiwashukuru kwa michango
wao waliyo ionyesha ndani ya klabu hiyo katika kipindi chote cha utumishi wao ndani ya klabu hiyo.
Wachezaji hao ni pamoja na Jabir Aziz(Stima), Ibrahim Mwaipopo, Malika Ndeule
na Omar Mtaki ambao wamemaliza mikataba yao na hawataongezewa mkataba mwingine.
Azam FC pia
imepokea na kuyakubali maombi ya wachezaji wake wawili, Samih Haji Nuhu na Luckson Kakolaki kustaafu kwa sababu mbalimbali.
Ibrahim Mwaipopo |
Nuhu anasumbuliwa na maumivu ya goti ambalo hana matumaini ya kupona
karibuni, wakati Kakolaki ameamua kustaafu ili achukue mafunzo ya
ukocha.
Klabu imempa ajira ya kudumu Nuhu katika moja ya viwanda vyake,
wakati Kakolaki ameingizwa kwenye benchi la Ufundi la akademi ya klabu.
Pia uongozi wa klabu hiyo umefikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na
mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ismail Kone ambaye alikuwa anamaliza
Novemba mwaka huu.
Pande zote mbili zimefikia makubaliano na mchezaji huyo amepewa haki zake na kurejea nchini mwao.
Tayari Azam fc imekamilisha usajili wa wachezaji wapya watatu, ambao ni
washambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, Ismaila Diarra kutoka Mali
na mzalendo Frank Domayo.
Usajili wa Kavumbangu na Diarra unafanya Azam iwe na wachezaji watano wa kigeni, wengine wakiwa ni Kipre Herman Tchetche na Kipre Michael Balou, ndugu wawili na pacha kutoka Ivory Coast na Mganda Brian Umony.
Azam chini ya kocha wake, Mcameroon Joseph Marius Omog imepanga kuboresha zaidi kikosi ili msimu ujao iweze kupata mafanikio zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea ubingwa wa Bara.
No comments:
Post a Comment