Brendan Rogers wa Liverpool |
Meneja wa Crystal Palace Tony Pulis na yule wa Liverpool Brendan Rodgers ni mameneja pekee wawili aliorodheshwa katika orodha fupi ya mameneja watakao wania tuzo ya msimu huu wa mwaka ya PFA.
Inawezekana inafaa zaidi kwani usiku huu watakuwa wanakutana uwanja wa Selhurst Park mchezo ambao una la kusema kuamua mbio za ushindi wa taji la Premier League.
Wekundu Liverpool wanahitaji ushindi kuijiongezea mwanya wa alama dhidi ya vinara wa sasa Manchester City, lakini kwao wao Palace wamekuwa katika kiwango safi cha uchezaji chini ya meneja Pulis.
Bosi huyo wa zamani wa Stoke City aliwaongoza vema mpaka kufikia kujinasua kutoka katika hatari ya kushuka daraja ambayo ilikuwa ikionekana tangu mapema mwa msimu.
Mameneja wote wawili wamefanya kazi nzuri na wamekuwa kivutio kulingana na uwezo na viwango vya vikosi vyao wanapokuwa uwanjani.
Ni vigumu kusema nani atashinda kwani kila mmoja ana weza kushinda na wana uwezo wa kufanya hivyo, lakini tunzo nyingi huwa zinakwenda kwa watu ambao wako juu ya msimamo wa ligi kuliko yule aliye chini ya msimamo huo na hivyo meneja wa Liverpool akionekana kupewa nafasi kubwa kuliko Pulis.
Tony Pulis wa Crystal Palace |
Endapo Rodgers atashinda ligi haitakuwepo nafasi kwa Pulis kushinda tunzo hiyo, na ushindi dhidi ya Palace usiku wa leo kwa Liverpool itakuwa pia imeongeza presha kwa Manchester City na ni mafanikio kuelekea kushinda kwa mara ya kwanza taji katika kipindi cha miaka 24.
Pengine mchezo huu unaweza kuamua nani atashinda tunzo ya meneja wa mwaka, kwani kuna mambo mengi zaidi ya matokeo ya mchezo wenyewe.
No comments:
Post a Comment