Hii ni taarifa ya ushuhuda wa wazi kabisa kuwa Louis Van Gaal anakwenda kuchukua nafasi ya kuingoza Manchester United .
Gazeti la kijerumani la Bild leo limeongoza na taarifa kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Thomas Muller anataka kuondoka kwa mabingwa wa ligi kuu ya nchini humo na kuungana na meneja mtarajiwa na ambaye ni hivi karibuni tu atathibtishwa na Old Trafford kuwa bosi mpya.
Van Gaal alifanya kazi na Muller katika kipindi chake cha miaka miwili ya kuingoza Munich (2009 mpaka 2011)
maarufu kama Bavarians na kumfanya mchezaji huyo wakati huo akiwa na umri wa miaka 19 kuwa katika wachezaji wa kikosi cha kwanza na kushinda taji la ligi katika msimu wake wa kwanza.
Gazeti la Bild limedai Muller anataka kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza baada kugundua heshima yake imeshuka chini ya meneja wake wa sasa Pep Guardiola ambaye amekuwa akimtumia kama mchezaji wa akiba.
Mtendaji mkuu wa Munich Karl-Heinz Rummenige ananukuliwa akisema
‘Kama mchezaji anajihisi hana amani ndani ya Bayern Munich, anapaswa kuja ofisini kwangu, halafu tuongelee juu ya hilo’
Louis Van Gaal anatarajiwa kutajwa na United kama bosi mpya wiki hii na akitarajiwa kuanza kazi rasmi ndani ya Old Trafford baada ya fainali ya kombe la dunia akikamilisha majukumu yake ya kuiongoza timu ya taifa ya Uholanzi kikamilifu.
Meneja huyo wa zamani wa Ajax na Barcelona atatakiwa kuwa na kiasi cha pauni milioni 150 ili kujenga upya kikosi cha United, huku mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Muller akithaminishwa kwa pauni milioni 35.
Mbali na Muller mwingine ambaye anahusishwa na kujiunga na United akitokea Bayern ni Toni Kroos.
No comments:
Post a Comment