KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 5, 2014

Hili ni kosi la Coastal Union lilishindwa kufurukuta msimu wa ligi 2013/2014. Nini tatizo?

Vifaa hivi vya Wagosi, kutoka kushoto Haruna Moshi 'Boban', Mbwana Kibacha, Abdi Banda, Juma Nyoso, Jerry Santo na Shaaban Kado. 

Naikumbuka Coastal kwa namna walivyo jitahidi kufanya usajili kamini kabla ya kuanza msimu uliomalizika wa 2013/2014 ikiwa na wachezaji hatari na wenye uwezo wa kuvutia na kutia moyo. 
 
Haruna Moshi 'Boban' Jerry Santo, Shabani Kado, Fikirini Suleiman, Hamadi Juma, Abdi Banda, Yusuf Chuma, Mbwana Kibacha, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Kenneth Masumbuko, Danny Lyanga.

Wengine Mansour Alawi, Ayoub Masoud, Marcus Ndeheli, Ayoub Semtawa, Mohammed Miraji, Crispian Odula, Mohammed Kipanga na wengine.

Nini kiliisibu kikosi hicho kushindwa kupata nafasi ya kuwakilisha nchini katika mashindano ya kimataifa ya vilabu barani Afrika chini ya kocha Yusufu Chipo aliyerithi mikoba kutoka kwa Hemedi Morocco?

 Kwa mfuatialiaji mzuri wa soka hapa nchini, bila wasiwasi atakuwa naye anajiuliza juu ya nini tatizo la timu hiyo kushindwa kufanya uzuri, kwani kama ni udhamini walikuwa nao kupitia kwa kambuni ya Binslum wauzaji wakubwa wa matairi haba nchini. Naomba maoni yako.
 

No comments:

Post a Comment