Inadhaniwa wazi kabisa kuwa mpango mzima umekamilika lakini Louis van Gaal
anasema hana uhakika kuwa atakuwa meneja mpya wa Manchester United.
Mduchi huyo anatarajiwa kuwa katika benchi la ufundi la Uholanzi katika michuano ijayo ya kombe la dunia huku pia taarifa zikiarifu kuwa ameshamalizana na United kwenda kuchukua nafasi ya umeneja Old Trafford baada ya fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
Akiongea wiki hii Van Gaal amesema bado hajakubali kujiunga na United na kwamba inawezekana ikasalia hivyo bila ya kuwa meneja wa klabu hiyo.
‘Sijafikia hatua hiyo bado[yaani ya kusaini mkataba],’ amesema van Gaal.
‘bado haiajawa wazi kama tutafikia hatua hiyo, tusubiri.
‘baadhi ya mambo yaliyokuwa yamependekezwa ni wazi siya kweli.’
United walikuwa wakitazamiwa kumtangaza Van Gaal wiki hii lakini taarifa zinasema kuwa suala hilo limeahirishwa kwani pande mbili hizo bado zinasuguana juu ya vifungu fulani ndani ya mkataba huo.
No comments:
Post a Comment