Jazba: Tyson Fury (kushoto) na Dereck Chisora (katikati) wakati wa kutambiana ana kwa ana ndani ya Manchester Printworks, pambano ni July 26.
|
Tyson
Fury na Derek Chisora walilazimika kutenganishwa na walinzi wakati wa majigambo yao ya ana kwa ana kuelekea pambano baina yao la kuwani mkanda wa uzito wa juu wa WBO maarufu kama 'Final
Eliminator' ambalo litapigwa July 26.
Wawili hao walikutana ana kwa ana wakibadilishana tambo kabla ya jazba kupanda kufuatia Fury kudai pambano hilo si la Chisora kushinda.
Chisora akaanza kupandishwa moto wa jazba kutoka kwa watu wa familia ya Fury waliokuwa pembeni ya jukwaa ambao kimsingi walitaka bondia huyo kutenda kosa nje kwa umati uliokuwepo ukumbini hapo.
Fury alidai kuwa alikuwa anakwenda kumchapa Chisora
Chisora ambaye kwasasa ana umri wa miaka 30 alishindwa kuvumilia kutokana na maneno ya kaka yake na Fury aliyekuwa pembeni ya jukwaa ambapo alilazimika kwa kumwita 'chubby'( yaani demu anayetafuta bwana) na kutumia maneno mengine 'f****** t***' wakati wawili hao wakipambana kwa vita ya maneno kabla ya mtangazaji(pundit) kutoka BoxNation Steve
Bunce kujaribu kuendeleza mahojiano yake.
Chisora
pia alikasirishwa na tuhuma za hivi karibuni za mpinzania wake Fury kuwa bondia huyo wa uzito wa juu anatumia madawa ya kuongeza nguvu 'anabolic steroids' ambazo ni kama kuweka mafuta ya taa kwenye moto.
Pambano baina yao litachezwa jijini Manchester ukumbi wa Phones 4 U Arena Jumamosi ya July 26 usiku ambao pia Billy Joe Saunders azichapa na Emmanuel
Blandamura uzito wa kati.
Last chance: Fury and Chisora will meet at the final world title eliminator on July 26 |
No comments:
Post a Comment