Ushindi : Rafael Nadal ametinga fainali ya Madrid Open final baada ya kumchapa Roberto Bautista 6-4 6-3 hapo jana. |
Rafael
Nadal ameendeleza mafanikio yake kuelekea kuchukua taji la michuano ya tenis ya Madrid
Open kufauatia matokeo ya kumtupa nje ya michuano hiyo mhispania Roberto Bautista kwa alama 6-4
6-3 hapo jana na kutinga fainali.
Nadal ambaye ndiye anayeshikilia namba moja kwa ubora duniani analikimbiza taji lake la jumla la 63 likiwa pia taji la 44 katika "clay court' yaani uwanja wa changarawe licha ya kwamba hakuwa katika kiwango bora mwaka huu, alipoteza katika hatua ya robo fainali katika michuano ya Monte Carlo na Barcelona.
Hata hivyo ameonyesha ustadi mkubwa mbele ya mashabiki katika katika mji mkuu wa Hispania ambapo mpaka sasa hajapoteza seti hata moja ikiwa ni pia anayatumia mashindano haya kama sehemu ya maandalizi yake ya kuendeleza rekodi yake ya kuchukua kwa mara ya tisa taji la French Open huko Roland
Garros mjini mwishoni mwa mwezi huu.
Ushindi wake wa nusu fainali dhidi ya Bautista unampeleka kwenye mchezo wa fainali leo dhidi ya ama nyota mwingine wa Hispania namba tano kwa ubora David Ferrer, ambaye alimchapa katika robo fainali ya Monte Carlo au anaweza kukutana na mjapani namba 10 kwa ubora duniani Kei Nishikori.
Nadal
anasema kiwango chake ni dhahiri kimeimarika baada ya Ijumaa kushinda dhidi ya raia wa Czech namba sita kwa ubora Tomas Berdych katika hatua ya robo fainali.
Bautista atakuwa akiingia katika orodha ya ubora wa wachezaji 30 baada ya kutinga nusu fainali ya Madrid Open
No comments:
Post a Comment