|
Luis Suarez akipambana na nahodha wake katika klabu ya Liverpool Steven Gerrard mjini Sao Paulo |
Mshambulizi wa Uruguay, Luis Suarez aliung'ata mkono
unaomlisha alipofunga mabao mawili na kuisaidia Uruguay kasajili
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uingereza katika mchuano wao wa kundi D,
huko Sao Paulo. Matokeo hayo yameiwacha Uingereza mguu nje mguu ndani ya
kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.
Hata ingawa mkufunzi wa Uingereza Roy Hodgson
hakubadilisha kikosi chake kutokana na kile kilichocheza dhidi ya Italia
huko Manaus katika mechi yao ya awali, alimpa Wayne Rooney nafasi ya
kucheza katikati, nyuma ya mshambulizi Daniel Sturridge.
Kufwatia kichapo cha 3-1 dhidi ya Costa Rica, Oscar Tabarez alifanya mabadiliko 5 katika kikosi kilichochuana na Uingereza.
Mwamuzi Carlos Velasco Carballo akiongea na Gerrard kufuatia kufanyiwa madhambi kwa Raheem Sterling
Suarez aliyekua na jeraha la goti pia alijumuishwa katika kikosi hicho.
Suarez aliupiga mpira wa kona ambao ulimpata
Hart akiwa hayuko tayari, hata hivyo aliweza kuutoa mpira huo nje na
kusababisha kona nyingine.
Nafasi nzuri ya Uingereza ya kupata bao,
ilikuja pale Sturridge alipoupiga mpira ambao uligusa mkono wake Diego
Godin naye refa wa mechihiyo Carlos Velasco akawapa waingereza mpira wa
adhabu katikati ya ya uwanja.
Rooney aliupiga lakini ukatoka nje, hata ingawa hatua chache tu.
Timu zote mbili zilipata nafasi nzuri na umiliki , bila kukamilisha mashambulizi .
Hata hivyo Rooney alikaribia kufunga bao lake la
kwanza katika michuano yote ya kombe la dunia ambayo ameshiriki katika
dakika ya 31.
Gerrard alikatishwa tamaa na matokeo ya kichapo kutoka kwa Uruguay
Shuti yake Steven Gerrard iliingia katika eneo la penalti la Uruguay
naye Rooney na Godin wakapigania mpira huo ambao Rooney aliupata kwa
kichwa ila tu uligonga mwamba wa lango la Uruguay .
Nicolas Lodeiro aliupata mpira katikati ya uwanja na akampisha Edinson Cavani.
Mchezaji huyo wa Paris Saint Germain alimpiga chenga Phil Jagielka na akampata Suarez aliyefunga kwa kichwa.
Hayo, katika dakika ya 39, Suarez akawapa La Celeste, bao la kwanza.
Kama walivyofanya dhidi ya Italia, Uingereza pia
ilishambulia muda mfupi baadaye. Rooney alimpa Sturridge pasi naye
akawapita walinzi wa Uruguay na kutoa mkwaju uliookolewa na , kipa wa
Uruguay Fernando Musclera.
Hata hivyo waingereza walikataa kufa moyo.
Dakika kumi na tano kabla mchuano kukamilika, Rooney alipata mpira kutoka kwa Glen Johnson naye akafunga bao la kusawazisha.
Bao lake la kwanza katika michuano yoyote ya kombe la dunia.
Timu zote mbili zilianza kutafuta bao la ushindi.
Mashabiki wa Uingereza walivumilia timu yao iliposhindwa na Uruguay
Mpira wake Musclera ulimfikia Suarez na mchezaji
huyo wa Liverpool akaupita ulinzi wa Uingereza na kufunga bao la pili
dhidi ya Hart zikiwa zimesalia dakika tano mechi kukamillika.
Uingereza bado ina matumaini ya kuendelea iwapo
wataishinda timu ya Costa Rica na kusubiri ikiwa matokeo ya mechi baina
ya Italia na Uruguay yatakuwa mazuri kwao.
Uingereza sasa watafurushwa kutoka kwenye kombe
la dunia Brazil 2014 iwapo wapinzani wao katika kundi hilo Costa Rica
watatoka sare ama kushinda Italia katika mechi yao ya pili itakayochezwa
Ijumaa.
No comments:
Post a Comment