KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, June 15, 2014

Ivory Coast yafungua milango kwa Afrika yaichapa Japan 2-1

Mshambuliaji wa  Ivory Coast akishangilia bao la ushindi akiwa na mkongwe  Didier Drogba.
Mipira miwili ya vichwa iliyopigwa na wachezaji Wilfried Bony na Gervinho ikiwa ni kwa kipindi cha muda wa sekunde 98 imezaa magoli mawili yaliyotosha kuwapa ushindi Ivory Coast dhidi ya Japan ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia wa kundi lao uliopigwa uwanja wa Recife.
The Elephants ilianza bila ya Didier Drogba lakini ilikuwa ni kama alikuwa amekalia magoli hayo katika benchi kwani kuingia kwake dakika ya 60 kulifungua nafasi muhimu zilizo zaa magoli mawili ya haraka ya Tembo.
Keisuke Honda akiandika bao utangulizi
 Japan ilitangulia kupata bao la utangulizi kupitia kwa Keisuke Honda goli zuri la dakika ya 16 huku Ivory Coast ikiendelea kupoteza nafasi nyingi za kufunga.