Kozi ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B
inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyodumu kwa wiki
mbili inafungwa kesho (Juni 20 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Makocha 26 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar
wameshiriki katika kozi hiyo chini ya wakufunzi wa CAF, Sunday Kayuni, Salum
Madadi wa Tanzania na Honory Janza kutoka Zambia. Ufungaji wa kozi hiyo unatarajiwa
kufanywa saa 5 asubuhi kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume.
Walioshiriki kozi hiyo ni Abdalla Mohammed Juma
(Zanzibar), Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke), Abdulmutik Haji
(Zanzibar), Aley Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein (Zanzibar), Dennis Kitambi
(Morogoro), Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe (Shinyanga), Fikiri Elias
(Arusha), Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar (Zanzibar), Juma Mgunda
(Tanga) na Kidao Wilfred (Ilala).
Wengine ni Maka Mwalwisi (Mbeya), Malale Hamsini Keya
(Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed Tajdin (Temeke), Mussa Furutuni
(Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar), Peter Mhina (Ruvuma), Said Mohamed
Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar), Salum Ali Haji (Zanzibar), Sebastian
Nkoma (Ilala), Wane Mkisi (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment