Kocha Mkuu mpya wa Yanga SC Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kulia ni msaidizi wake Leonado Neiva |
Kocha mbrazil Marcio Maximo leo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa
ajili ya kuwatumikia Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya
Young Africans pamoja na msaidizi wake Leonadro Neiva ambao wamesema
wamekuja kuisaidia Yanga iweze kufanya vizuri kwenye michuano
mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Maximo
amesema anajiskia furaha sana kurudi kufanya kazi Tanzania, kwani watu
wake ni wakarimu, wapenda mpira hivyo anaona kama yupo nyumbani japo
awamu hii ni kwa majukumu ya ngazi ya klabu tofauti na awali alipokua
ngazi ya Taifa.
Nimekuja kufanya kazi na Yanga, nawashukuru
viongozi wake kwa kuamua kuniamini na kunipa nafasi hii, wamenifuatilia
kwa awamu tatu mfululizo na hatimaye safari hii wamefanikiwa kunipata
kwa kushirikiana na wakala wangu Ally Mlei sasa kazi ni moja tu kuijenga
Yanga.
"Jumatatu naanza kazi moja kwa moja pamoja na msaidizi
wangu Neiva kwa kushirikiana na kocha wa kikosi cha U-20, wachezaji
waliopo na wachezaji wa kikosi cha U20 watakua wakifanya mazoezi pamoja
alisema" Maximo".
Natambua
tuna wachezaji wengi katika timu za Taifa mbalimbali ikiwemo ya
Tanzania (Taifa Stars), Uganda (The Cranes) na Rwanda (Amavubi) ambao
wapo wanayatumikia mataifa yao, na punde watakapomaliza majukumu hayo
wataungana nasi kwa maandalizi.
Kuhusu Kaseja yale yalishapita,
najua ni kipa mzuri mwenye uwezo na uzoefu wa kutosha na kipindi hiki
najivunia kuwa na makipa watatu wenye uwezo mzuri, Yaliyopita
Yameshapita yalikuwa ni timu ya Taifa na sasa tumekutana Yanga kazi yetu
ni moja tu kuifanya klabu iwe kwenye hadhi ya Kimataifa zaidi.
Naye
kocha msaidizi Leonado Neiva amesema tumekuja kufanya kazi, kwa
kushirikiana na wachezaji waliopo kutoka sehem mbambali barani Afrika na
Amerika tutapata mchanganyiko mzuri wa uchezaji.
Wakala wa Maximo
Barani Afrika Bw Ally Mlehi kwa upande wake amewaomba wapenzi,
wanachama na washabiki wa Yanga kuwa wavumilivu kwani soka ni tofauti ni
chai ambayo ukikoroga sukari tu unasikia utamu, badala yake wanapaswa
kuwapa muda makocha na baadae wataaona matunda yake.
No comments:
Post a Comment