KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 12, 2014

Pepe Reina kuidakia Arsenal msimu ujao, Wenger atoa pauni milioni 5

Reina's future is currently up in the air (Picture: Getty)
Pepe Reina yuko katika mawindo ya Arsena(Picture: Getty)

Arsenal wako tayari kuweka dau la pauni milioni 5 mezani kumchukua mlinda mlango asiyekuwa tena na nafasi katika klabu ya Liverpool Pepe Reina.
Reina amekuwa akielezwa kuihama Anfield kiangazi lakini Napoli klabu aliyokuwa akiichezea kwa mkopo imeshindwa kuweka mezani pesa ya kumchukua moja kwa moja.
Alikaririwa wiki akisema amekuwa katika sintofahamu ya hatima yake ya baadaye licha ya Arsenal kutaka kumaliza fununu za kumchukua na kumpa nafasi London ya kaskazini.
Kwa mujibu wa taarifa za kupenyeza ambazo Rockerspots imezinasa ni kuwa meneja Arsene Wenger anataka kupenyeza pauni milioni £5 kwa ajili ya huduma yake na yuko katika nafasi nzuri ya kumpata.
The Gunners wanasaka mlinda mlango wa pili baada ya Lukasz Fabianski kuelekea Swansea, Reina alikuwa katika rada yao kwa muda sasa.