KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 6, 2014

Usajili bongo: David Luhende ajiunga na Mtibwa Sugar

Davidi Luhende mwenye jezi ya kijani na njano ajiunga na Mtibwa Sugar.
Baada ya kuachwa na Yanga Afrika hatimaye mlinzi wa kushoto David Charles Luhende amejiunga na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Luhende ambaye ameitumikia klabu ya Yanga kwa misimu miwili na kufanikiwa kuvaa medali ya Ubingwa msimu wa 2013/2014 alitangazwa kuachwa na Yanga hivi karibuni na kuibua maswali mengi kwa wadau wa soka nchini juu ya sababu ya Yanga kumucha mlinzi huyo ambaye bado mdogo na uwezo ni mkubwa kiasi cha kuitumikia hata timu ya Taifa.

Davidi Luhende akiwa na jezi ya timu Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Uganda
Akiongea na Rockesports msemaji wa Mtibwa Thobias Kifaru amethibitisha kusajiliwa kwa Luhende na kwamba kocha wa kikosi hicho Mecky Mexime ndiye aliyependekeza kuchukuliwa kwa Luhende ili aweze kuongeza nguvu ndani ya kikosi chake ambacho kinahitaji mlinzi wa kushoto.
Luhende aliitwa kwa mara kwanza katika kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' mwaka jana kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe alipotimkia Ulaya kwenye majaribio ambapo alionyesha kiwango cha juu katika kumudu vema nafasi ya ulinzi wa kushoto katika kikosi cha timu ya Taifa.