KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 6, 2014

Salum Swedi Kusi astaafu rasmi kucheza soka

Salum Swedi Kusi
 Beki na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Swedi maarufu kama Kusi, ametangaza kustaafu kabisa kucheza soka na kwamba ameamua kuanza maisha mengine nje ya mchezo huo.

Uamuzi wa Kusi umefuatia kumalizika kwa mkataba wake na wakata miwa wa Turiani Manungu, timu ya Mtibwa Sugar.

Akiongea na Rockersports Sued aliyezaliwa Disemba 3 1980, amesema maamuzi yake yamekuja baada ya kuona kuwa amecheza soka kwa muda mrefu na kutoa mchango wa kutosha katika vilabu mbalimbali hapa nchini pamoja na timu ya Taifa Taifa Stars, hivyo imefika wakati sasa kuwaachia vijana wengine wapate nafasi hiyo ya kuonyesha vipaji vyao.

 Swedi ameitumikia Mtibwa kwa miaka saba kwa vipindi viwili tofauti. Alijiunga na Mtibwa mwaka 2006 mpaka 2009 kabla ya kuondoka na kujiunga na Azam fc msimu wa 2010/2011.
Kumbuka pia Swedi aliwahi kuichezea Yanga kuanzi mwaka 2001 mpaka 2005.

Amekuwa mlinzi wa kati wa kutumaini wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010 kabla ya kustaafu mwenyewe kwa hiari yake wakati huo Stars ikiwa chini ya kocha wa sasa wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo.
Salum Swedi anastaafu kabisa kucheza soka akiwa na umri wa miaka 34
 
Salum Swedi Kusi akiwa na jezi ya Mtibwa akipambana na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Didier Kavumbagu ambaye kwasasa amejiunga mabingwa soka Tanzania bara Azam fc.

No comments:

Post a Comment