KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 5, 2014

Pablo Armero aliyeng'ara akiwa na Colombia anamezewa mate na Arsenal na Southampton

Pablo Armero
Arsenal na Southampton wameripotiwa kutaka kusajili mlinzi wa kushoto wa Colombia Pablo Armero msimu huu wa kiangazi wakati ambapo tayari mchezaji mwenyewe anataka kurejea Premier League msimu ujao.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 27 anayechezea Udinese amekuwa akicheza kwa mkopo West Ham katika nusu ya pili ya msimu ambapo amecheza michezo mitano.
Ameonyesha kiwango cha juu katika kikosi cha Colombia katika kombe la dunia ambapo ameripotiwa kumezewa mate na vilabu vingi nchini England ikiwemo Arsenal na Southampton