KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, July 5, 2014

Pengine Neymar angeparalyse kama angegongwa juu kidogoNyota wa Brazil  Neymar ilikuwa kidogo tu ange-paralyse endapo angegongwa nchi moja juu ya zaidi ya eneo lililogongwa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Colombia ambao Brazil waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 usiku wa jana Ijumaa.

Mshambuliaji huyo alilazimika kubebwa katika machela kunako dakika ya 88 huku akilia kwa maumivu makali baada ya kugongwa na Juan Zuniga wa Colombia na mlinzi huyo hakuweza kupewa adhabu yoyote kwa tukio hilo.


Daktari wa timu Rodrigo Lasma, ameimbia televisheni ya Brazil akisema kuwa mchezaji huyo amevunjika uti wa mgongo katika eneo la vertebra na kwamba atakosekana katika michezo iliyosalia ya fainali hizo ambapo atahitaji upasuaji.

Lakini kwa mujibu wa taarifa nyingine kutoka nchini Brazil zinasema kuwa mshambuliaji huyo wa Barcelona aligongwa na Zuniga nchi moja chini ya eneo ambalo kama angegongwa juu zaidi basi paralyse.