Shirikisho la soka duniani FIFA huenda likaichukulia hatua kali Nigeria kwa kuingilia kati usimamizi wa kandanda.
Mabingwa hao wa Afrika huenda wakapigwa marufuku
ya kushiriki mashindano yeyote ya soka yanayo andaliwa na FIFA baada ya mahakama nchini
humo kufuta kazi maafisi wote wa shirikisho la soka nchini humo.
Waziri wa michezo wa Nigeria Tammy Danagogo alimteua Lawrence Katiken kuwa msimamizi mkuu wa NFF.
Fununu kutoka nchini humo zinasema kuwa matokeo duni ya timu hiyo hayakusaidia hali mbaya ya uhusiano na serikali ya nchi hiyo.
Super Eagles iliambulia kichapo cha 2-0 mikononi
mwa Ufaransa katika raundi ya pili ya kombe la dunia na hivyo
kufungashwa virago.
Mahakama ya jimbo la Plateau ilitoa amri ya kupinga uongozi wa Aminu Maigari, na kamati yake nzima.
Matukio kama hayo katika miaka ya awali yalisababisha marufuku ya FIFA kwa Nigeria sawa na Kenya.
Nigeria ilinusurika kupigwa marufuku ya
kushiriki mashindano ya kimataifa mwaka wa 2010 baada ya serikali
kutishia kususia mashindano yote kwa miaka miwili kwa niya ya kuijenga
upya kikosi chake kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia Afrika
Kusini..
Nigeria ilifuzu kwa hatua ya pili huko Brazil kwa mara ya tatu katika historia ya mashindano ya kombe la dunia .
Nigeria ilikuwa imewahi kufuzu kwa kombe a dunia katika miaka ya 1994 na 1998.
Mwaka uliyopita Nigeria ilitawazwa mabingwa wa
Afrika huku kikosi chake cha vijana wasiozidi umri wa miaka 17
wakishinda kombe la dunia .
No comments:
Post a Comment