Equatorial Guineanje ya michuano ya Afrika |
Equatorial Guinea imeondolewa nje ya mashindano ya kuwania tikiti ya kuwania ubingwa wa Afrika mwakani huko Morocco.
Kamati inayosimamia michuano hiyo imeipata taifa
hilo na hatia ya kumchezesha mchezaji kinyume na kanuni za shirikisho
la soka duniani FIFA.
Kamati hiyo simamizi iliipata E.
Guinea na hatia ya kumshirikisha mzaliwa wa Cameroon Thierry Fidieu
Tazemeta, katika ushindi wao wa mkondo wa kwanza dhidi ya Mauritania
tarehe 17 Mei.
Hakuna ushahidi uliotolewa kudhibitisha kuwa Tazemeta alikuwa kabadili Uraia .
Mauritania ilikuwa imeuliza kudhibitishwa kwa uraia wa mchezaji huyo katika mkondo wa kwanza ilipoibuka mshindi wa 1-0.
Equatorial Guinea hata hivyo ilipuuza madai
hayo na ikamshirikisha katika mechi ya pili ambayo E .Guinea iliibuka
na ushindi mkubwa wa 3-0 .
Kufuatia kauli hiyo Mauritania imerejeshwa mashindanoni na sasa itakabiliana na Uganda katika mkondo wa mwisho wa kufuzu.
Mwaka uliopita Equatorial Guinea ilipoteza mechi
mbili kwa sababu sawa na hizo katika mechi ya kufuzu kwa dimba la dunia
la Brazil,2014.
No comments:
Post a Comment