Katika historia za kukutana Argentina imeshinda mara
tatu katika mara nne zilipokutana wakati Ubelgiji ikishinda mara moja
mwaka 1982 kwa kuifunga Argentina kwa goli 1 - 0 katika hatua ya
makundi.
Argentina ilitolewa mara tatu ya mwisho katika
hatua ya robo fainali. Ilipoteza dhidi ya Ujerumani mwaka 2010 na dhidi
ya Uhalanzi mwaka 1998 na baadae ikatolewa na Ujerumani mwaka 2006 kwa
mikwaju ya penalti.
Ukiachilia mbali kuondolewa kwa
mikwaju ya penalti, Argentina haijawahi kushinda kwenye hatua ya robo
fainali tangu ilipoifunga England mwaka 1986 magoli 2 -1.
Tegemeo la Argentina kwa sasa Lionel Messi
ambaye amefunga au kusaidia kufungwa kwa magoli matano kati magoli saba
Argentina iliyofunga katika kombe la dunia la mwaka huu 2014.
Magoli matatu ambayo Messi aliyafunga manne aliyafunga nje ya kisanduku cha kumi na nane.
Kwa upande wa Ubelgiji hii ni mara ya pili kwao
kufikia hatua ya robo fainali. Mara ya mwisho iliifunga Uhispania mwaka
1986 kuingia hatua ya nne bora.
Argentina |
Ubelgiji |
01 Romero 04 Zabaleta 23 Basanta 14 Mascherano 15 Demichelis 02 Garay 22 Lavezzi 06 Biglia 09 Higuaín 10 Messi 07 Di María Wachezaji wa Akiba03 Campagnaro05 Gago 08 Pérez 11 Rodríguez 12 Orión 13 Fernández 17 Fernández 18 Palacio 19 Álvarez 20 Agüero 21 Andujar |
01 Courtois 02 Alderweireld 05 Vertonghen 06 Witsel 15 van Buyten 04 Kompany 11 Mirallas 08 Fellaini 17 Origi 07 De Bruyne 10 Hazard Wachezaji wa Akiba03 Vermaelen09 Lukaku 12 Mignolet 13 Bossut 14 Mertens 16 Defour 18 Lombaerts 19 Dembélé 20 Januzaj 21 Vanden Borre 22 Chadli 23 Ciman |
No comments:
Post a Comment