KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, July 4, 2014

Grand Malt kukabidhi vifaa vya udhamini wa ligi kuu ya Zanzibar hapo kesho

Innocent Meleck wa kwanza mratibu wa udhamini wa Grand Malt
Wadhamini wa ligi kuu ya soka ya visiwani Zanzibar kampuni ya bia nchini TBL kupitia kinywaji cha Grand Malt, kesho wanatarajia kukabidhi vifaa vywa michezo kwa viongozi wa klabu zitakazoshiriki katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa visiwani humo msimu wa mwaka 2014-15.

Mratibu wa shughuli za udhamini wa ligi ya visiwani Zanzibar Innocent Meleck amesema TBL kupitia Grand Malt pia watasaini mkataba mpya na viongozi wa ZFA ambao utajumuisha maboresho ya udhamini wa ligi ya visiwani humo.

Meleck amesema ana hakika ndoa ya ZFA pamoja na Grand Malt itaendelea kudumu kutokana na mazuri ambayo yanaonekana tangu walipojitosa kuidhamini ligi ya visiwani Zanzibar.

Amesema udhamini wa Grand Malt hii leo umewapa faraja mashabiki wa soka wa Zanzabar ambao wanaona wachezaji wao wanavyoitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania Taiofa stars, kufutia aviwango vyao vya soka kupiga hatua siku hadi siku.