KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

Joachim Low: Licha ya kuwafunga Brazil kwa mvua ya magoli sasa nahisi huruma

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low amesema pamoja na furaha iliyokithiri kambini kwake kufuatia matokeo ya kihistoria waliyoyapata kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali usiku wa kuamkia hii leo, bado anahisi huruma kwa wapinzani wao Brazil.

Low, amesema anajihisi huruma kutokana na wenyeji Brazil kuambulia kibano ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya soka lao, hali ambayo anadhani huenda ikawa ni zaidi ya maumivu kwa mashabiki nchini humo.

Amesema alijisi unyonge pale alipokutana na kila shabiki ama afisa wa Brazil katika korido ya kuelekea kwenye vumba vya kubadilishia, na yeye kama binaadam alingia huruma na kutamani kulia lakini ujasiri wa ushindi mkubwa alioupata ulimpa nafasi ya kutembea kifua mbele.

No comments:

Post a Comment