KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

Lowasa akutana na Rais wa Simba Evance Aveva na kumtaka afanye mambo kadhaa. ( Chanzo ni mtandao wa Liwazozito.blogspot.com)

Waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa akutana na Rais wa Simba na kunene machache.
WAZIRI Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ameutaka uongozi mpya wa Simba kutolipiza kisasi au kufukua maovu ya uongozi uliopita, badala yake ujikite katika kuweka mikakati ya kuendeleza klabu. Lowassa alisema hayo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam jana alipotembelewa na Rais mpya wa Simba, Evans Aveva. Lowassa amemtaka Aveva kuunganisha wanachama wa Simba kwa manufaa ya soka ya Tanzania. Aidha aliwataka viongozi wa klabu kubwa nchini kusajili zaidi wachezaji wa
nyumbani na kuachana na tabia ya kukimbilia kusajili wachezaji wa kigeni kwani hiyo inadhoofisha uimara wa timu ya taifa.
Lowassa alitolea mfano timu ya taifa ya Uingereza ilivyofanya vibaya katika Kombe la Dunia, akisema inatokana na klabu nyingi za ligi kuu ya nchi hiyo kuwa an wachezaji wengi wa kigeni kuliko wale wa ndani. Kwa upande wake,  Rais huyo wa Simba alisema uongozi wake umejipanga kuwekeza katika soka ya vijana ili kupunguza gharama za kusajili wachezaji wapya kila msimu. Pia alimueleza Lowassa kuwa wanatarajia kufungua hosteli katika kipindi kifupi kijacho katika eneo jipya la klabu hiyo huko Bunju. Alisema awamu ya pili ndiyo itakuwa ya ujenzi wa uwanja ambapo alimuomba Lowassa kukubali mualiko wa kufanya harambee ya kukusanya fedha za ujenzi wa uwanja huo wakati ukifika.

No comments:

Post a Comment