KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

Mshike mshike wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2014/15 utaanza kutimua vumbi lake Septemba 20.

Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza mabadiliko ya kuanza kwa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15 ambayo ilikuwa imepangwa kuanza kutimua Augusta 24 mwaka huu.

Taarifa iliyotumwa katika dawati la mtandao wa Rockersports na afisa habari na mawasilino wa shirikisho hilo Bonface Wambura inaeleza kwamba mshike mshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2014-15, sasa utaanza kutimua vumbi lake Septemba 20 mwaka huu.

Sababu kubwa iliyoelezwa na TFF ya kusogeza mbele kuanza kwa ligi ya msimu ujao ni kutaka kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.
Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.
Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.

No comments:

Post a Comment