KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 9, 2014

MAXIMO SASA KUTETA NA WANAHABARI KILA IJUMAA, AKERWA KULISHWA MANENO

Marcio Maximo kocha wa Yanga ajiwekea utaratibu wa kuongea na waandishi wa habari
Kocha mkuu wa timu ya Young Africans SC Mbrazil Marcio Maximo amesema atakua akiongea na waandishi wa habari kila siku ya Ijumaa asubuhi mara tu baada ya mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ili kuwapa nafasi na fursa ya kumuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na maandalizi ya kikosi chake msimu ujao. Akiongea na mtandao rasmi wa klabu ya Young Africans Maximo amesema, ameamua kufanya hivyo ili kupunguza kuwepo taarifa tofauti kuhusiana na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake katika maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015. "Unajua utendaji wa kazi umebadilika, nafasi yangu kwenye klabu na nilipokua timu ya Taifa ni tofauti, hivyo nimekubaliana na uongozi na umeniruhusu kuwa naongea na vyombo vya habari kwa pamoja kila siku ya Ijumaa mara tu baada ya mazoezi ya asubuhi "alisema Maximo
 Maximo ameanza kazi ya kukinoa kikosi cha Young Africans tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwatuvia wapenzi, washabik na wanachama ambao wamekua wakijitokeza kwa wingi kushuhudia ufundishaji wa kocha huyo mwenye mvuto mkubwa kwenye soka la Tanzania.